Jeshi la polisi mkoani Morogoro kushirikiana na jeshi la zimamoto na uokoaji na wananchi wa mtaa wa Mzambarauni kata ya Mwembesongo Manispaa ya Morogoro wamefanikikiwa kuwathibiti wananchi wa eneo hilo waliotaka kuchota mafuta baada ya Lori lenye namba za usajili T. 257 EAU kuanguka.
Mwenyekiti wa mtaa huo amesema baada ya kupata taarifa za tukio hilo alitoa taarifa kwenye vyombo vya usalama na kufanikiwa kuthibiti kundi hilo la wahalifu.
Mwakilishi wa Jeshi la Zimamoto na uokoaji Mkoa Morogoro Daniel Myala amesema Lori hilo lilibeba mafuta aina ya dizeli zaidi ya Lita elfu arobaini hadi Sasa bado haijafahamika mafuta kiasi gani yaliyomwagika.
Amesema Dereva wa Lori amejeruhiwa na amekimbizwa hospitali Kwa ajili ya matibabu
Ikumbukwe kuwa katika eneo hilo Miaka mitano iliyopita Lori la mafuta lilianguka na watu wakachota mafuta kisha badae kuwaka moto na kusababisha vifo vya watu zaidi ya mia Moja.