Mke wa Rais wa zamani Nchini Marekani Michelle Obama hatahudhuria kuapishwa kwa Donald Trump wiki ijayo, kwamujibu wa Taarifa iliyotolewa na ofisi yake Jumanne,
Mumewe Barack Obama atakuwepo tarehe 20 Januari ingawa, kulingana na taarifa iliyotolewa na ofisi ya Rais wa zamani hakuna maelezo ambayo yametolewa kwa nini Michelle Obama alikwepa kuapishwa kwa Bw Trump. Pia hakuhudhuria mazishi ya Rais wa zamani Jimmy Carter wiki iliyopita.
Uamuzi wa kuacha kuhudhuria kuapishwa rasmi kwa Trump ni kuvunja desturi kwa sherehe hiyo, ambapo marais wa zamani na wake zao kwa kawaida hushiriki.
Rais wa zamani George WBush na Laura Bush watahudhuria uzinduzi huo, ofisi yake ilisema, na Rais wa zamani Bill Clinton na Hillary Clinton pia watakuwepo.
Wanawake wengine wa zamani wa kwanza, akiwemo Hillary Clinton na Laura Bush, wote walihudhuria hafla ya Carter.
Michelle Obama amezungumza waziwazi kuhusu chuki yake dhidi ya Trump, ambaye amemshutumu kwa kuweka usalama wa familia yake hatarini kupitia matamshi yake.
Ikumbukwe kuwa Trump hakuhudhuria kuapishwa kwa Rais Joe Biden mnamo 2021 huku kukiwa na madai ya uwongo ya rais mteule kwamba alishinda uchaguzi wa 2020.