Thomas Mulliez, Rais wa Moët Hennessy kwa Ulaya, Mashariki ya Kati na Afrika, yupo nchini Tanzania wiki hii ili kuonyesha kuimarika kwa uwepo wa kampuni hiyo kiuchumi na kitamaduni.
Ziara hii inakuja kutilia mkazo imani ya chapa hiyo ya kifahari duniani katika nchi ya Tanzania kama sehemu inayokuwa kwa kasi na kwa haraka zaidi katika soko lililosheheni bidhaa za vinywaji hivyo maarufu zaidi duniani.
Tanzania imekuwa mojawapo ya sehemu za uwekezaji zenye mvuto mkubwa zaidi Afrika Mashariki, ikiwa na mazingira ya kisiasa ya utulivu, mageuzi ya biashara ya kisasa, na uchumi unaotarajiwa kukua kwa asilimia 5.7% mwaka 2025, kwa mujibu wa Benki ya Dunia. Moët Hennessy imekuwa sehemu inayochagiza maisha ya kifahari nchini, ikileta bidhaa kama Moët & Chandon na Hennessy kwa wateja mbalimbali na kuchangia katika maendeleo ya Ukuaji wa Jiji la Dar es Salaam na kuwa kituo kikubwa cha burudani nchini Tanzania.
Mnamo mwaka 2024, Moët Hennessy ilianza sura mpya katika operesheni zake nchini Tanzania kupitia ushirikiano na Mohan’s Oysterbay Drinks Limited (MODL), msambazaji maarufu wa ndani mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka 40. Ushirikiano huu umeongeza wigo wa soko wa Moët Hennessy, kuboresha uwezo wa usafirishaji na kuimarisha nafasi ya kampuni kama kichocheo cha nguvu za kiuchumi. Kutokana na uwepo huu kumeongeza uongezeko wa ajira, kusaidia wasambazaji wa ndani, na kukuza kubadilishana uzoefu, ushirikiano huu ni uthibitisho wa kujitolea kwa chapa hii maarufu katika ukuaji wa Tanzania.
Zaidi ya biashara, Moët Hennessy ina nia kubwa ya kushirikiana na jamii na kusherehekea Vipaji vya Kitanzania. Kupitia mpango wa Hennessy Cypher 2024, kampuni imeweka jukwaa kwa wasanii wa hip-hop wa Afrika kuonyesha ubunifu wao na kufikia watazamaji wa kimataifa. Miongoni mwao, msanii wa Kitanzania Young Lunya alishiriki, na jukwaa hili lilichagiza kupandisha na kuongeza ushawishi wa sanaa yake kimataifa. Vivyo hivyo, Juma Jux naye alikuwa miongoni mwao akionyesha ushirikiano kati ya Hennessy na tamaduni za Afrika, akionesha ubora wa Kitanzania kwenye jukwaa la kimataifa. Kupitia ushirikiano wake na Hennessy, Juma Jux ameudhuria matukio muhimu kama Michezo ya NBA nchini Ufaransa mwaka 2023 na Ligi ya Basketball ya Afrika ya Rwanda mwaka 2024, akiangazia uhusiano mkubwa wa Hennessy na michezo na tamaduni za Afrika.
Moët Hennessy pia hushirikiana na wabunifu maarufu wa ndani kama mbunifu Mtani Bespoke na mjasiriamali Nancy Sumari, ambao wanaonyesha ubunifu na ufanisi wa tamaduni za Kitanzania. Ushirikiano huu unaimarisha kujitolea kwa kampuni ya kuimarisha vipaji vya ndani na kutangaza tamaduni za Kitanzania duniani.
Ziara ya Thomas Mulliez imekuja kimkakati huku ikiweka bayana malengo na maono ya Moët Hennessy kwa soko la Tanzania. Kwa kutumia utaalamu wake wa kimataifa na kushirikiana na wadau wa ndani, kampuni inatarajia kutoa huduma bora huku ikichangia katika uchumi na kulinda Tamaduni za Kitanzania.
Wakati Tanzania inajiandaa kwa ukuaji wa kiuchumi na kutambulika duniani, Moët Hennessy iko tayari kuimarisha uhusiano wake sokoni kuchagiza ukuaji huo, lakini pia imejizatiti kuanzisha ushirikiano wa kibunifu, na kudumisha nafasi yake kama mdau muhimu katika kuchagia uwepo wa maisha ya kifahari nchini Tanzania.