Vyanzo vingi vya habari vya Urusi vinasema Korea Kaskazini itashiriki katika gwaride la Siku ya Ushindi huko Moscow mwezi Mei. Tukio hilo linaashiria ushindi wa uliokuwa Umoja wa Kisovieti dhidi ya Nazi ya Ujerumani.
Vyanzo hivyo viliiambia NHK kwamba ushiriki wa jeshi la Korea Kaskazini katika sherehe za Ushindi wa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia mnamo Mei 9 tayari umeshaamuliwa.
Wanasema wanatarajia makumi ya maafisa wa Korea Kaskazini watashiriki.
Vyanzo vingine vya kidiplomasia vinasema bendi ya kijeshi ya Korea Kaskazini itashiriki katika tamasha la muziki jijini Moscow mwishoni mwa mwezi Agosti.
Vyanzo vya habari vinabainisha kuwa jeshi la Korea Kaskazini litakuwa linashiriki katika matukio haya kwa mara ya kwanza.
Jana Jumatano, Waziri wa Ulinzi wa Urusi Andrei Belousov, alisema kuwa vikosi vya kijeshi kutoka nchi rafiki 19 vimealikwa kwenye gwaride la Siku ya Ushindi.
Alisema kuwa tayari nchi 10 zimethibitisha ushiriki wao, lakini hakutaja majina ya nchi hizo.