Mwanamke mmoja wa Australia anashikiliwa na jeshi la polisi baada ya kudaiwa kumwekea sumu mtoto wake mwenye umri wa mwaka mmoja sumu na kumrekodi kisha kupost ili kupata michango na wafuasi mtandaoni.
Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 34 kutoka Queensland, ambaye hakutajwa jina, amefunguliwa mashtaka baada ya kushikiliwa na jeshi la polisi nchini humo
Inadaiwa alimpa mtoto huyo “dawa kadhaa ambazo hazijaidhinishwa na za duka la dawa” bila kibali cha matibabu kati ya Agosti na Oktoba mwaka jana, Polisi wa Queensland walisema.
Polisi walimtaja mtoto huyo kama mtu wake wa karibu lakini hawakuthibitisha ikiwa mtoto huyo ni binti yake.
Mtoto huyo alipokuwa katika “shida na maumivu makali”, polisi wanadai kuwa mwanamke huyo “alirekodi na kuchapisha video” zake mtandaoni ili “kushawishi michango ya fedha na wafuasi mtandaoni”.
Inspekta wa upelelezi Paul Dalton aliwaambia wanahabari mwanamke huyo anayedaiwa kuwalaghai wafadhili zaidi ya $60,000 (£30,500) kupitia GoFundMe.
Mwanamke huyo pia alichukua hatua makini kuficha madai ya kupewa sumu, ambayo yaliripotiwa tu kwa polisi wakati madaktari waliporipoti madhara dhidi ya mtoto huyo alipolazwa hospitalini.
Kufuatia uchunguzi, mwanamke huyo alishtakiwa mnamo Januari 16 na makosa matano ya kutoa sumu kwa nia ya kudhuru, makosa matatu ya kujitayarisha kufanya uhalifu kwa vitu vya hatari, na kila moja la mateso, kutengeneza nyenzo za unyonyaji wa watoto na utapeli, polisi walisema.