Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo inatarajia kusikiliza kesi ya kusambaza taarifa za uongo kupitia mtandao wa X ( Twitter) inayomkabili mwanasiasa mkongwe Dkt.Wilbroad Slaa.
Awali mahakama hiyo ilikwama kusikiliza kesi hiyo baada ya Upande wa Jamhuri na Utete kutojua alipo mshtakiwa huyo na pia kutokujua sababu za yeye kutokuletwa mahakamani.
Kesi hiyo nambari 993 ya mwaka 2025 inatarajiwa kusikilizwa mbele ya Hakimj Mkazi Mkuu, Beda Nyaki.
Ilidaiwa kuwa Dk Slaa alitenda kosa hilo Januari 9 mwaka huu ndani ya Jamhuri a Muungano wa Tanzania kupitia mtandao huo wa kijamii , kupitia jukwaa lililosajiliwa kwa jina la Maria Salungi Tsehai @MariaSTsehai kwa lengo la kupotosha umma.
Ilidaiwa kuwa, kupitia jukwa hilo Dk Slaa alichapisha ujumbe uliosomeka ‘wakubwa wametafutana, nikisema wakubwa namaanisha mwamba na Samia, na wala hatuna maneno ya kumung’unya,….na kimsingi wamekubaliana, Suluhu Samia amekubali atatoa pesa, Suluhu Samia amekubali ataongeza nguvu ya pesa ni dhahili atatoa pesa…hizo ni hela za Watanzania wanazichezea Samia na watu wake.
‘Samia toka muda mrefu haangaikii tena maendeleo ya nchi anahangaikia namna ya kurudi Ikulu, na namna yake ya kurudi Ikulu ni kwa njia hizo kama kumsaidia mtu kama Mbowe’ ,wakati akijua taarifa hizo ni za uongo.