Mshambulizi wa klabu Eintracht Frankfurt na timu ya taifa ya Misri Omar Marmoush, amekamilisha uhamisho kwenda Manchester City ya Uingereza na anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya ndani ya saa 32 zijazo.
Marmoush anakuwa Mmisri wa kwanza kuchezea Manchester City ya Pep Guardiola na amekuwa na kiwango bora mno kwa siku za karibuni kwenye Ligi ya Ujerumani na mashindano mengine kwa klabu ya Frankfurt.
Nyota huyo hatari, amefunga mabao 20 na assist 14 msimu huu kwenye Bundesliga, Europa League na kwenye DFB Pokal akiwa ni miongoni mwa nyota wenye namba nzuri na kubwa zaidi msimu huu barani Ulaya.
Marmoush atatambulishwa na City muda wowote kutoka sasa ili kuongeza nguvu katika safu ya ushambuliaji inayoongozwa na Erling Haaland ambayo msimu huu inasuasua ukilinganisha na msimu uliopita.