Rais wa Korea Kusini aliyeondolewa madarakani Yoon Suk Yeol amekaa usiku wake wa kwanza kuzuiliwa kama mfungwa kabla ya kesi yake katika Kituo cha Kizuizi cha Seoul baada ya mahakama kutoa hati rasmi ya kumweka kizuizini kwa hadi siku 20.
Alikuwa rais wa kwanza aliye madarakani kukamatwa nchini Korea Kusini wiki jana na alizuiliwa kwa saa 48 za awali za kuhojiwa, kutokana na uchunguzi wa iwapo alifanya uasi na azma yake ya kutangaza sheria ya kijeshi mnamo Desemba 3.
Baadae alipigwa picha kwa ajili ya kutambuliwa na alifanyiwa “ukaguzi wa kina”, afisa wa huduma ya urekebishaji alisema.
“Haijalishi wewe ni rais, kila mtu anapigwa picha kwa asilimia 100 wakati unaingia kwenye kituo,” alisema ofisa huyo ambaye alikataa kutajwa jina kwa sababu hakuwa na mamlaka ya kuzungumza na vyombo vya habari.
Ukaguzi wa kimwili sio tu kuangalia afya bali pia “kama unaficha kitu,” alisema afisa huyo.
Yoon alikamatwa wiki iliyopita chini ya waranti iliyoruhusu mamlaka kumshikilia kwa hadi saa 48, iliyotolewa na mahakama wakati mshukiwa katika kesi ya jinai anakataa kujibu wito au kutoa ushirikiano.
Chini ya sheria za Korea Kusini, kizuizini ni mchakato tofauti ambapo wachunguzi wanaweza kumshikilia mshukiwa kwa hadi siku 20, kwa mahojiano zaidi ikiwa kuamua kuna sababu za kuamini kuwa mshukiwa anaweza kujaribu kuvuruga ushahidi au mashahidi au ni hatari ya kukimbia.