Kila rais mpya huanza sura mpya katika historia ya Marekani na wakati huu ambapo Donald Trump anatawazwa huko Washington DC yenye baridi leo, atakuwa na matumaini ya kuanzisha enzi mpya kwa nchi hiyo.
Trump ameahidi mabadiliko pamoja na kuchukua hatua siku ya kwanza tu atakapo ngia madarakani ikiwemo kuirudisha TikTok kwa watumiaji wa nchi hiyo.
Katika mkutano mkubwa wa hadhara mjini humo siku ya Jumapili, Trump alisema atatia saini msururu wa maagizo ya utendaji ndani ya muda mfupi baada ya kuapishwa, yanayohusu masuala kuanzia kufukuzwa kwa wahamiaji na kufuta haki za watu waliobadili jinsia.
Lakini hata kama urais wake ukianza kwa kishindo kikubwa, bado kuna maswali kuhusu kitendo cha pili cha Trump kitakuwaje.
Uapisho huo unafanyika katika Ikulu ya Marekani mjini Washington DC leo na Donald Trump na Makamu wake JD Vance watashiriki sherehe za kuapishwa saa 12:00 kwa saa za huko (17:00 GMT), ambapo watakula kiapo kupokea ofisi.
Trump ameahidi kusuluhisha “kila tatizo” linaloikabili Marekani na kuweka amri kadhaa mpya katika siku zake za kwanza za urais wake.
“Katika historia ya Marekani, tutakuwa na siku bora zaidi ya kwanza ya urais, wiki bora zaidi ya kwanza na siku bora zaidi 100 za kwanza kuwahi kushuhudiwa,” alisema Trump.