Papa Francis ametoa maoni juu ya kile raismteule wa Marekani Donald Trump kuhusu mipango ya kuwafukuza wahamiaji nchini humo .
Papa alisema mipango ya Donald Trump ya kuwafukuza wahamiaji kwa wingi itakuwa ni “fedheha,” alipokuwa akizingatia ahadi za rais ajaye wa Marekani karibu muongo mmoja baada ya kumwita “si Mkristo” kwa kutaka kujenga ukuta kando ya Marekani na Mexico.
“Kama ni kweli, hii itakuwa fedheha, kwa sababu inawafanya masikini wasio na chochote kulipa bili” kwa tatizo hilo, Francis alisema. “Hii haitafanya jambo jema! Hii sio njia ya kutatua mambo. Sivyo hivyo mambo yanavyotatuliwa.”
Trump, ambaye anaapishwa siku ya Jumatatu, aliwashukuru watu wengi kuwa kuchagua mtu sahihi kwenye kampeni yake na ameahidi safu ya maagizo ya siku ya kwanza ya kurekebisha sera ya uhamiaji.
Hii si mara ya kwanza kwa Trump kuzungumzia hili kwani wakati wa kampeni yake ya kwanza ya urais, mwaka wa 2016, Francis aliulizwa kuhusu mipango ya Trump ya kujenga ukuta kwenye mpaka wa Marekani na Mexico.
Akizungumza baada ya kuadhimisha Misa mpakani, Francis alisema kwa shauku kwamba mtu yeyote anayejenga ukuta kuzuia wahamiaji “sio Mkristo.”