Rapa wa Marekani, Nelly ametetea uamuzi wake wa kutumbuiza kwenye sherehe za kuapishwa kwa Donald Trump baada ya kutokea pingamizi.
Nyota huyo wa Hot in Herre anatarajiwa kutumbuiza pamoja na The Village People at the Liberty Inaugural Ball, kwenye sherehe rasmi inayoashiria kurejea kwa Trump kwenye Ikulu ya White House.
Nelly alikosolewa mtandaoni baada ya kutajwa kuwa angetokea lakini akasema ni “heshima” kutumbuiza rais “bila kujali ni nani yuko ofisini”. “Ninaheshimu ofisi,” alisema wakati wa mazungumzo ya moja kwa moja na rapa Willie D. “Hii sio siasa.
Siasa, kwangu, imekwisha. [Trump] alishinda! Yeye ni rais. Yeye ndiye amiri jeshi mkuu wa kile ningependa kusema ni nchi bora zaidi duniani.”