Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam inawashikilia watuhumiwa wawili Fred Rajabu Chaula na Bashir Richard Chaula kwa tuhuma za kula njama na kumuua Regina Rajabu Chaula mwenye miaka 62 mkazi wa Bahari beach wilaya ya Kinondoni
Akitoa taarifa hiyo kamanda wa kanda Maalum ya Dar es salaam SACP Jumanne Murilo amesema kuwa mwanamke huyo alikuwa na kesi za madai mahakama kuu Divisheni ya Ardhi dhidi ya watuhumiwa na watu wengine na alipotea ghafla na hakuonekana tangu tarehe 13 ya mwezi december 2024.
Aidha ameongeza kuwa baada ya ufatiliaji wa kina katika maeneo mbalimbali na watu makachero wa polisi walilazimika kubomoa shimo la maji machafu lilikuwa karibu na nyuma aliyokuwa anaishi marehemu na kukuta mwili wa Regina chaula ukiwa umeanza kuharibika.