Rais wa Urusi Vladimir Putin siku ya Jumatatu alimpongeza Rais anayekuja wa Marekani Donald Trump kwa kurejea Ikulu ya White House, anapotarajiwa kushika madaraka yake baada ya sherehe za kuapishwa baadaye leo.
“Tunaona kauli ya Rais mpya wa Marekani aliyechaguliwa na wanachama wa timu yake kuhusu nia ya kurejesha mawasiliano ya moja kwa moja na Urusi, iliyoingiliwa bila kosa letu na utawala unaoondoka.
“Pia tunasikia kauli yake kuhusu haja ya kufanya kila kitu kuzuia vita vya tatu vya dunia. Bila shaka, tunakaribisha hali kama hiyo na tunampongeza Rais mteule wa Marekani kwa kuchukua madaraka,” Putin alisema wakati wa mkutano wa Baraza la Usalama la Urusi.
Akikariri kwamba Moscow iko tayari kufanya mazungumzo na utawala mpya wa Marekani kuhusu vita vinavyoendelea vya Ukraine, Putin alisema jambo muhimu zaidi katika suala hili ni kuondoa sababu kuu za mzozo huo.