Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, mkoani Songwe, Ester Mahawe, amezikwa leo na maelfu ya watu nyumbani kwake Ngaramtoni ya chini jijini Arusha,huku akimwagiwa sifa za kuwa mstari wa mbele kwa utetezi wa wanaume.
Ester, alifariki Januari 14 mwaka huu majira ya saa 1:30 asubuhi katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC iliyopo mkoani Kilimanjaro na kuacha mume na watoto watatu na watoto sita wa kuwalea pamoja na wajukuu tisa.
Marehemu alifariki akiwa anarudi Arusha Januari 13 mwaka huu kutoka Hospitali ya Lugalo Dar es Salaam na akiwa njian hali yake ilibadilika na kulazimika kupelekwa Hospitali ya KCMC ambako alifariki.
Akizungumza jana kwenye ibada ya mazishi ya Ester, Ngaramtoni ya Chini jijini Arusha, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Dk.Festo Dugange, ametoa pole kwa niaba ya Rais Samia Suluhu Hassan, huku akiwasihi wengine kuacha hadithi iliyo njema kama aliyoiacha ya utetezi wa wanaume.
“Marehemu anasifa nyingi ila mwinyi alishasema maisha ya mwanadamu ni hadithi tu, ila jitahidi kuwa hadithi iliyo njema ili wanaobaki waendelee kuyasimulia, huyu ndugu yetu Ester ametuachia hadithi njema ya kuwatetea wanaume na kuacha upendo kwa kila mtu,”amesema.
Amesema alifanya kazi kwa ufanisi na kuwa mfano bora kwa wenzake waliopewa nafasi na Rais, hivyo kila mmoja ahakikishe anabaki kuwa hadithi iliyo njema kwa wale anaowaongoza.
“Kila dhamana mnayopewa muifanyie kazi kwa bidii na maarifa ya hali ya juu hilo ndilo aliloliacha marehemu na alisisitiza hata mwanamke ukipata V8 hesimu mwanaume,amesema