Shirika la Afya Duniani (WHO), limeipatia Tanzania shilingi bil. 7.55, ili kudhiti na kukabiliana na ugonjwa wa Marburg nchini.
Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Dk. Tedros Adhanom Ghebreyesus, ameyasema hayo, leo, alasiri, Ikulu ya Chamwino, Dodoma, akizungumza na kwenye mkutano na Rais Samia Suluhu Hassan.
Awali, akizungumza katika mkutano huo, Rais Samia amesema tangu kuwapo taarifa kuhusu uwapo wa ugonjwa Marburg mkoani Kagera, seriikali imekwishachukua hatua kwa kufanya uchunguzi eneo husika.
Kadhalika, rais amesema kikosi cha dharura kimechukua hatua kwa kufanya uchunguzi, ili kupata majibu na kuthibitisha.
Amesema kwamba ujio wa Mkurugenzi huyo pamoja na ujumbe wake, ni ishara ya ushirikiano kati ya Tanzania na WHO, katika kukuza nguvu ya kikazi kwa pamoja.
“Tangu kuwapo minong’ono kuhusu Marburg mkoani Kagera, serikali imekwishachukua hatua…Tanzania imeboresha maeneo ya kinga pamoja na kuimarisha huduma za afya ya msingi, kuanzia ngazi ya chini.
“Ninamshukuru Dk. Tedros na timu yake na nina furasa kukutana katika kipindi hiki cha changanoto za kiafya barani Afrika,” amesema Rais Samia.
Kwa upande wake Dk. Tedros, amesema WHO itaendelea kutoa ushirikiano ikiwamo katika sula hilo, baada ya kuwapo taarifa kuhusu ugonjwa huo na kwamba Tanzania ilikwishachukua hatua mbalimbali kama vile kuwa na maabara tembezi.