Tundu Antipas Lissu hatimayee ndie mwenyekiti rasmi wa CHADEMA taifa.
Lissu alitangazwa mshindi alfajiri Jumatano, Januari 22, baada ya shughuli ya upigaji kura uliofanyika usiku kucha katika mkutano wa wajumbe wa taifa wa chama hicho, jijini Dar es Salaam.
”Ushindi huu ni wetu sote!” aliandika Lissu katika ukurasa wake wa X muda mfupi baada ya matokeo kujulikana.
Mgombea Uenyekiti Freeman Mbowe, alimpongeza Tundu na wenzake (akiwemo John Heche) kwa ushindi katika Uchaguzi uliofanyika kuanzia jana hadi usiku wa kuamkia leo
Mbowe ameandika kupitia ukurasa wake wa X (zamani Twitter) kuwa “Nimepokea kwa mikono miwili maamuzi ya uchaguzi wa Mkutano Mkuu wa Chama chetu CHADEMA uliohitimishwa leo asubuhi January 22, 2025, nampongeza Tundu Lissu na wenzake kwa kuaminiwa kutwikwa jukumu la Uongozi wa Chama, nawatakia kila la kheri katika kukipeleka mbele Chama chetu”
Taarifa kutoka kwenye vyanzo vya vya kuaminika ndani ya chumba cha kuhesabia kura zinadai kuwa Lissu amepata kura zaidi ya 500 sawa na asilimia 51, wakati kwa upande wa Heche nae akipata kura zaidi ya 500 ambazo ni sawa na asilimia 57 ya kura zote.
Kupitia AyoTV Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA ambaye amegombea Uenyekiti wa CHADEMA Taifa ametoa kauli yake ya kwanza baada ya mpinzani wake Mwenyekiti wa sasa Freeman Mbowe kukubali kushindwa kupitia ukurasa wake wa twitter