Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amepongeza juhudi za kidiplomasia za Rais wa Marekani Donald Trump kupata kuachiliwa kwa mateka na makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya Israel na Hamas baada ya takriban miezi 15 ya vita.
“Kulikuwa na mchango mkubwa wa diplomasia imara ya rais mteule wa wakati huo wa Marekani,” anasema katika Kongamano la Kiuchumi la Dunia huko Davos, Uswisi.
Maafisa wa Kiarabu waliliambia gazeti la Times of Israel wiki iliopita kwamba wanaamini kuwa Trump na mjumbe wake Steve Witkoff walihusika na mafanikio yaliyosababisha makubaliano hayo