Utitiri wa Kodi kwa wafanyabiashara ni moja ya changamoto kubwa inayosababisha kukwepa ulipaji Kodi stahiki kwa kundi hilo na kwamba jambo hilo si tu linadhohofisha maendeleo ya wafanyabiashara hao kuendesha biashara zao lakini pia linaikosesha Serikali kupata kodi inayostahili.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Chemba ya Wafanyabiashara na Kilimo Mkoa wa Morogoro Mwadhine Mnyanza wakati wa kikao tume ya Rais ya maboresho ya Kodi kilichofanyika mjini .Morogoro ambapo amesema wafanyabiashara hukumbana na changamoto mbalimbali zikiwemo wingi wa kodi, kubwa hasa katika sekta zinazokuwa kibiashara jambo linalopelekea kufikia hatua ya kukwepa kodi.
Myanza amesema ni vizuri Serikali ikaweka chombo Kimoja cha kukusanya Kodi ambayo itakuwa rafiki Kwa wafanyabiashara ,lakini Kila taasisi kukusanya Kodi kwenye biashara Moja inadhoofisha maendeleo Yao .
Anasema kutoka ana changamoto hiyo inawalazima wengine kukwepa Kodi ,kukimbia madeni na Kufunga biashara na kusababisha kukosekana kwa mapato.
Kwa upande wake Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mkoa wa Morogoro amesema katika eneo muhimu sana katika kuboresha mazingira ya biashara hapa Nchini ni kuangalia suala la wingi wa kodi ambalo linaweza kuwavutia wawekezaji wengi, hivyo ameiomba Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kushirikiana katika kutoa mafunzo kwa wafanyabiashara juu ya umuhimu wa kulipa kodi.
Mwenyekiti wa Tume ya Rais ya Maboresho ya kodi Balozi Mwanaid Maajar amesema, kilio cha wengi ni utitiri wa kodi unaotokana na uchache wa walipa kodi huku Mamlaka husika zikiwa zinaelekeza nguvu zake za kudai kodi sehemu chache ili kupata kodi jambo ambalo linamrudisha nyuma mfanyabiashara kwa sababu ya kulipa kodi nyingi.
Balozi huyo amesema.lengo la Tume hiyo kuwa kupokea malalamiko, changamoto na mapendekezo ili kuboresha mazingira ya kufanyia biashara na kuangalia namna ya kurahisisha utaratibu wa wafanyabiashara kupata leseni, kulipa tozo na kulipa kodi kwa urahisi.
Amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano w Tanzania Dokta Samia Suluhu Hassan ameanzisha tume hiyo Ili iweze kutatua changamoto hizo hivyo wafanyabiashara wakae meza Moja na mamlaka husika Ili kumaliza changamoto hizo.