Mnyama aina ya Kiboko aliyewahi kuwa tishio kwa kuuwa Ng”ombe watatu kuharibu Mazao ya wananchi na Kujeruhi Mtu Mmoja katika kijiji cha Itare Kata ya Katoma Halmashauri ya wilaya ya Geita Mkoani Geita ameuwawa na Askari wa wanyamapori .
Akizungumza Baada ya kuuwawa kwa mnyama huyo Bi. Avelina Hoja amesema mnyama huyo amekuwa akiwasumbua sana na kupelekea kuuwa ng’ombe watatu , kujeruhi Mtu mmoja na kuharibu mazao ya wananchi hali ambayo ilikiwa ikiwapa hofu katika maeneo yao wanayoishi.
“Changamoto kubwa hapa ni hawa wanyama tunaangaika kwa takribani miaka mitano wametuharibia mazao wametuharibia watoto wetu pia hatuchoti maji kwa uhalisia tunahangaika sana inapofika mida ya jioni kwenda kuchota maji , ” Mwananchi Avelina Hoja.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Itare Halmashauri ya wilaya ya Geita, Michael Kongoro amekiri wananchi wako kusumbuliwa na mnyama huyo kwa kipindi cha miaka 5 huku akiwashukuru TAWA kwa kuona kilio chao na kuja kumdhibiti Mnyama huyo.
Afisa Wanyamapori msaidizi Daraja la pili kutoka kutoka Mamlaka ya Usimamizi wanayama pori Tanzania (TAWA) Sefu Marambo amethibitisha kuuwawa kwa mnyama huyo mkali huku akiwataka wananchi kutopanda mazao yanayoendanda na mnyama huyo kama chakula chake pamoja na kuweka tahadhari wanapokuwa wanaenda kuoga ziwani.