Naibu mjumbe wa Urusi katika Umoja wa Mataifa amejibu vitisho vya kiuchumi vya Rais wa Marekani Donald Trump dhidi ya Moscow.
Hapo awali, rais wa Marekani alisema ataweka ushuru na vikwazo “kama hatutafanya ‘dili’ hivi karibuni” la kuvimaliza vita vya muda mrefu sasa.
Dmitry Polyanskiy amesema Ikulu ya Kremlin ingehitaji kuona kile ambacho Trump anafikiria kuhusu makubaliano hayo kabla ya kuendelea.
“Sio suala la kumaliza vita tu,” Polyanskiy aliiambia Reuters.
“Ni suala la kwanza kabisa la kushughulikia sababu kuu za mgogoro wa Ukraine.”
Aliendelea: “Kwa hiyo tunapaswa kuona nini maana ya dili hili katika uelewa wa Rais Trump,yeye hahusiki na kile ambacho Marekani imekuwa ikifanya Ukraine tangu 2014, na kuifanya ‘anti-Russia’ na kujiandaa kwa vita na sisi, lakini ni katika uwezo wake sasa kukomesha sera hii mbovu.”