Kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Camillus Wambura, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, DCP Wilbroad Mutafungwa, amekabidhi Bendera ya Taifa kwa Kikosi maalum cha mbinu na silaha (SWAT), kinachoelekea nchini Rwanda kushiriki mashindano ya vikundi maalum vya kupambana na ugaidi yanayofanyika January 2025.
Mashindano hayo yatahusisha mapambano ya karibu, ulengaji shabaha na vikwazo yakihusisha nchi 14 za ukanda wa mashiriki mwa Afrika EAPCCO.
Akikabidhi Bendera hiyo, Kamanda Mutafungwa amewataka washiriki kuzingatia nidhamu, weledi, haki, na uadilifu pamoja na kujituma ili kuliletea Taifa ushindi.
Mkuu wa msafara wa kikosi hicho, Mrakibu Msaidizi wa Polisi ASP. Aizack Mwakisisile, amesema wamejiandaa vya kutosha na wanamatumaini ya kurejea nchini na ushindi.