MAKAMU wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) anayeshughulikia masuala ya nishati na mabadiliko ya hali ya hewa, Dk Kevin Kariuki amesema zaidi ya marais 25 na mawaziri wa fedha na nishati 60 wa Afrika watashiriki mkutano wa nishati utakaofanywa Dar es Salaam Januari 27 hadi 28, mwaka huu.
Aidha, viongozi wengine wa kimataifa watashuhudia wakuu wa nchi za Afrika wakikubaliana kusaini Mpango Mahususi wa Nishati wa Afrika, awamu ya kwanza utakaozishirikisha nchi 14.
Nchi hizo ni Tanzania, Malawi, Chad, Nigeria, Burkina Faso, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Niger, Liberia, Msumbiji, Madagascar, Zambia, Mali, Ivory Coast na Mauritania.
Alisema hayo jana Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya mkutano huo unad[1]haminiwa na Benki ya Dunia, AfDB na washirika wengine wa maendeleo kuhakikisha watu milioni 300 Afrika wanafikiwa na umeme ifikapo mwaka 2030.
Dk Kariuki alisema mkutano huo ni muhimu kwani utakutanisha wakuu wa nchi na viongozi wengine ambao baada ya kujadiliana, watasaini Azimio la Dar es Salaam linaloweka makubaliano yaliyofikiwa kutekelezwa kuhusu mkutano huo muhimu.
“Hadi sasa marais zaidi ya 25 na mawaziri wa fedha na nishati zaidi ya 60 wa Afrika wanaku[1]tana hapa na tutashuhudia viongozi hao wakikubaliana na kuingia mkataba wa kuwezesha lengo la kusambaza umeme kwa watu milioni 300 kabla ya 2030 kufikiwa,” alisema Dk Kariuki.
Alisema Benki ya Dunia na AfDB, Aprili mwaka jana walikubaliana kuwa haiwezekani wananchi wa Afrika wakaendelea kuishi katika upungufu wa umeme hivyo wakaamua kuja na mpango huo wa kuziwezesha nchi hizo kusambaza umeme kwa takribani wananchi milioni 300.
Alisema makubaliano hayo yanasimamiwa na nguzo kuu tano ambazo ni kuongeza uzalishaji na ku[1]wekeza katika miundom[1]binu kwa kuzingatia ush[1]indani, kuongeza miradi ya muunganiko wa mataifa ili kupunguza gharama za kusafirisha umeme.