Rais wa Marekani Donald Trump amesema anapanga kuwasiliana na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un baada ya kurejea Ikulu ya White House.
Trump aliulizwa kuhusu mipango yake kwa Kim wakati wa mahojiano Alhamisi na kama “atawasiliana”.
“Nitafanya, ndio. Alinipenda,” Trump alisema.
Trump na Kim walikuwa na uhusiano mkubwa usio wa kawaida wakati wa muhula wa kwanza wa rais madarakani kwa mataifa mawili ambayo hayakuelewana tangu Vita vya Korea miaka 70 iliyopita.
Trump hapo awali alielezea uhusiano wao kama “mzuri sana” na amemtaja Kim kama “mtu mwerevu” kwenye vyombo vya habari.
Wakati wa muhula wake wa kwanza madarakani, Trump alikutana na Kim mara tatu tofauti kati ya 2018 na 2019.
Mnamo mwaka wa 2019, aliweka historia kama rais wa kwanza wa Marekani aliyeweza kuzuru Korea Kaskazini tangu mapigano ya 1953 yalileta mwisho wa Vita vya Korea.