Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa amesema watalii Milion 1,863,108 (1.8) wametwmbelea hifadhi za Taifa ( TANAPA) Kwa kipindi cha mwaka 2023/2024 ikiwa ni ongezeko la watali 244,570 ukilinganisha na mwaka 2022/2023 ambapo watalii 1,618,538 (Mil. 1.6)
Msigwa amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika hifadhi ya Taifa Mikumi mkoani Morogoro akieleza mafanikio ya Serikali kwemye sekta mbalimbali.
Msigwa amesema ongezeko hilo limechagizwa na filamu ya The Royal Tour ambayo iliongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta Samia Suluhu Hasaan .
Aidha amesema Serikali inaendelea kuboresha miundombinu mbalimbali Kwenye sekta ya Utalii ikiwemo viwanja vya Ndege,malazi, na Barabara.
Ameongeza Kwa kusema Serikali imeendelea kutatua Migogoro ya ardhi katika ya hifadhi na Vijiji ambapo katika hifadhi ya Taifa Tarangire na Kijiji cha Kimotorok,hifadhi ya Taifa Serengeti ja Vijiji 7 vya wilaya ya Serengeti,hifadhi ya Taifa Ruaha na Mbarali,hifadhi ya Taifa Mahale na Kijiji cha Kalilani.
Pia amesema wakazi zaidi ya 3500 wa kata ya Nyatwali Wilayani Bunda mkoani Mara wamelipwa fidia Ili eneo hilo liwe sehemu ya hifadhi ya Taifa Serengeti ambapo eneo hilo linaukibwa wa ekari 14,250.
Pia Kupitia TANAPA Serikali imekusanya Bil 410.6 ikilinganishwa na Bil 382.3 ambazo zilikadiriwa Kwa mwaka wa fedha 2023/2024.