Rais wa Marekani Donald Trump amesema Microsoft ni miongoni mwa kampuni zinazofikiria kununua hisa za TikTok ili jukwaa hilo liepuke kupigwa marufuku kwa misingi ya usalama wa taifa.
Alipoulizwa Jumatatu ikiwa Microsoft ilikuwa katika mazungumzo ya kuinunua programu hiyo maarufu ya kushiriki video, Trump alisema: “Ningesema ndio.”
Trump alisema kulikuwa na “maslahi makubwa ndani ya TikTok” lakini alikataa kutoa orodha kamili ya makampuni ya Marekani ambayo yangependa kuinunua.
“Ninapenda vita vya zabuni kwa sababu unafanya mikataba yako inakuwa bora,” Trump aliwaambia waandishi wa habari alipokuwa akisafiri kutoka Miami hadi Washington, DC
Microsoft ilikataa kutoa maoni na TikTok haikujibu maswali mara moja.
TikTok iliingia gizani kwa muda mfupi nchini Marekani mnamo Januari 18 ili kutii sheria inayoamuru kwamba kampuni mama ya China ya ByteDance iondoke au kuona imepigwa marufuku.
Trump alisimamisha utekelezwaji wa sheria hiyo kwa siku 75 muda mfupi baada ya kuingia madarakani ili kuupa utawala wake muda wa kutafuta suluhu mbadala ya marufuku hiyo.