Roma wanavutiwa na kiungo wa kati wa Manchester United Casemiro huku wakitafuta mbadala wa Leandro Paredes, kulingana na Sky nchini Italia.
Nia ya klabu hiyo ya Italia kwa kiungo huyo wa Kibrazili inakuja huku kukiwa na sintofahamu kuhusu mustakabali wa Paredes, huku ripoti za hivi punde zikimuhusisha Muargentina huyo na uwezekano wa kurejea Boca Juniors.
Kocha wa Roma Claudio Ranieri ana nia ya kuendelea kumshikilia Paredes na atajaribu kumshawishi kuahirisha mipango yake ya kuondoka.
Casemiro, ambaye ameshindwa kudumisha kiwango chake Manchester United msimu huu, amezidi kujipata katika nafasi ya pili chini ya kocha mpya Ruben Amorim.
Mbrazil huyo mwenye umri wa miaka 32 amecheza mechi mbili pekee katika mechi tisa zilizopita za Premier League, na hivyo kuchochea uvumi kuhusu mustakabali wake Old Trafford.
Licha ya nia ya Roma, Fabrizio Romano amesema kuwa Casemiro anatarajiwa kusalia Manchester United hadi angalau 2025.