Neymar amekubali kurejea Santos takriban miaka 12 baada ya kuachana na timu ya Brazil, rais wa klabu hiyo Marcelo Teixeira alisema Jumanne.
Mshambulizi huyo wa Brazil alithibitisha mapema kwamba kandarasi yake na klabu ya Al-Hilal ya Saudi Arabia ilikuwa imevunjwa kwa makubaliano ya pande zote mbili. Alikuwa na majeraha katika klabu ya Al-Hilal, ambapo alicheza mechi saba pekee na kufunga mara moja.
Neymar mwenye umri wa miaka 32 alishinda mataji sita akiwa na klabu yake ya utotoni Santos, ikiwa ni pamoja na kombe la Copa Libertadores mwaka wa 2011. Santos ni mji ulio ufukweni nje ya São Paulo.
“Ni wakati (wa kurejea), Neymar. Ni wakati wa wewe kurudi kwa watu wako. Nyumbani kwetu, kwa kilabu mioyoni mwetu, “Teixeira alisema katika mitandao yake ya kijamii. “Karibu kijana wetu Ney! Kijana wa Vila (Belmiro, uwanja wa Santos). Rudi kuwa na furaha tena na shati nyeupe na nyeusi. Taifa la Santos linakungoja kwa mikono miwili.”
Neymar, ambaye aliwahi kusifiwa kama mmoja wa wachezaji bora zaidi duniani, alitumia muda mwingi nchini Saudi Arabia akiwa nje ya uwanja kutokana na jeraha la ACL alilolipata akiichezea Brazil Oktoba 2023.