Tanzania na Burundi zimesaini mkataba wa ujenzi wa Reli ya Kisasa SGR Kilomita 282 kutoka Uvinga mpaka Musongati nchini Burundi kwa gharama ya Sh. Trilioni5. ambapo inaelezwa kuwa mradi huo unatarajiwa kuwa kichocheo cha shughuli za uchumi na kijamii baina ya nchi zote mbili.
Akizungumza jijini DSM Waziri wa Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa amewataka Shirika la Reli Tanzania TRC kusimamia ujenzi wa Reli hiyo kwa viwango vya kimataifa vya ubora pamoja na kusimamia bajeti iliyopangwa.
Aidha Mbarawa mewataka TRC kuhakikisha wanatoa ajira kwa wananchi wanaoishi pembezoni mwa mradi huo.
Kwa upande wake Waziri wa Miundombinu wa Burundi, Captain Dieudonne Dukundane amesema Nchi ya Burundi iko tayari kusimamia Mkandarasi aliyepewa kazi ya kujenga mradi huo ili ukamilike kwa wakati na kuanza kufanya kazi.