Jamii imetakiwa kutambua umuhimu wa kuchukua risiti za kielectroniki pindi wanapo nunua bidhaa ili kushiriki vyema katika ulipaji wa kodi kwa maendeleo ya taifa.
Hayo yamezungumzwa na Shaga Gagunda Ofisa Elimu kwa Mlipa kodi na mawasiliano kutoka Mamlaka ya mapata Tanzania TRA
Mkoa wa Iringa wakati akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari Mwembetogwa iliyopo Manispaa ya Iringa na kubainisha kuwa ni wajibu wa mfanyabiashara kutoa risiti pindi afanyapo mauzo pasina kuangalia mauzo aliyoyafanya.
Gagunda amesema kuwa ikibainika mnunuzi hajadai risiti atakabiliwa na adhabu ya faini ya shilingi elfu 40 na muuzaji kwa kutotoa risiti adhabu yake ni faini ya million 2 na isiyozidi million nne kwa kukwepa kulipa kodi.
“…tukumbuke kwamba kuna adhabu kwa kushindwa kudai risiti kwako mnunuzi ambayo ni shilingi elfu 40 au asilimia 20 ya kodi iliyokwepwa na kuna adhabu ya kutotoa ni asilimia 20 ya thamani ya bidhaa iliyouzwa bila risiti au shilingi milioni mbili lakini hiyo adhabu haitakiwa kuzidi milioni 4 kwa kosa moja…”amesema gagunda
Wakizungumza mara baada ya kupata elimu ya umuhimu wa kudai risiti wanafunzi wa shule ya sekondari mwembetogwa wameishukuru TRA kwa kuwafikisha elimu hiyo na sasa wametambua umuhimu wake.
Bakari mbaga ni Mwalimu katika shule ya sekondari mwembetogwa ametoa wito wa kufunguliwa TRA klabu mashuleni ili kupata mabalozi watakaohamasisha jamii kutambua umuhimu wa kutoa na kudai risiti katika makazi yao.
“…elimu hii waliyoipata wanafunzi itawasaidia katika maisha yao ya kila siku kwani ni muhimu sana kufika katika shule mbali ili watoto watambue wakitumwa kununua bidhaa hawatakiwi kuchukua bila risiti hivyo mamlaka hii ifungue club za kodi vijana wafundishwe masuala ya kodi na wawe mabalozi watokapo…” amesema mbaga