Ni siku ya Burudani kwa wapenzi wa Muziki wa Dance nchini ambapo Bendi zaidi ya 10 zinakutana viwanja vya leaders Dar Es salaam kufurahia Muziki huo kupitia tamasha maalumu la Muziki wa Dance lilopewa jina la Kadansee la Mama Samia ambalo limeandaliwa na Baraza la Sanaa la Taifa BASATA
Katibu Mkuu wa BASATA Dkt Kedmond Mapana amesema ni siku ya kihistoria ya Muziki huo ikiwa na malengo adhimu ya kuurudisha Muziki wa dance kwenye chati zake na kuendelea kuenzi Muziki huo ambapo Bendi Zaidi ya 10 zitakutana leo viwanja vya leaders Dar es Salaam kuperfom na kubadilishana uzoefu tofauti tofauti
“Ni siku pekee sana leo haijawahi kutokea Kwenye Muziki wa Dance nchini, Kadansee la Mama Samia linaenda kuandika historia kubwa sana Bendi Zaidi ya 10 zipo leo hapa Leaders Club, watu waje kufurahia huu Muziki kutakua na starehe ya kutosha” Dkt Mapana