Kuelekea kuadhimisha siku ya Kuzaliwa ya Chama Cha Mapinduzi CCM, Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi Kata ya Msasani wameungana pamoja katika Dua maalum pamoja na kutoa msaada kwa wahitaji lengo Kuombea kheri ya kuzaliwa na kutimiza miaka 48 ya Chama cha Mapinduzi.
Akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kukabidhi mahitaji muhimu kwa Zahanati na Shule, Katibu wa Tawi la Umoja wa Wanawake Kata ya Msasani Bi, Mwajuma Bwaru amesema UWT Msasani ni muhimu kuendelea kutoa mahitaji muhimu kwa wahitaji kwani itasaidia kupunguza changamoto zinazoepukika.
” Uwt Msasani leo tumekuwa na jambo hili muhimu Tumetembelea Shule za Sekondari na Shule za Msingi pamoja na Zahanati ya Mikoroshini Msasani kwa kuwaletea mahitaji maalumu kama Taulo Za Kike, Dawa za Mbu, Pampers za Watoto wa Changa na Vingine vingi lengo ni kusapoti kazi zinazofanywa na Serikali ya Rais Samia” Amesema Katibu.
Hata hivyo Naye Mwakilishi wa Shule ya Msingi Msasani B Mwalimu Neema Poneka amewashukuru Umoja wa Wanawake CCM kwa zawadi hizo kwani ilikuwa ni mahitaji yao makubwa kwa muda mrefu sasa itapunguza utoro kwa Wanafunzi wa Kike Shuleni.