Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi ameleeza kuwa Serikali iko tayari kushirikiana na Madhehebu ya Imani zote kuhubiri Amani ,kudumisha Upendo na Umoja ndani ya Jamii kwani ndio Msingi wa mambo yote ya Maendeleo katika kila nyanja.
Rais Dk.Mwinyi ameyasema hayo alipozungumza na Askofu Mkuu wa Kanisa la Kilutheri Tanzania KKKT Dkt.Askofu Alex Gehaz Malasusa na ujumbe aliofuatana nao Waliofika Ikulu Zanzibar.
Aidha Rais Dk.Mwinyi Mwinyi amefahamisha kuwa Taasisi za dini zimekuwa na Mchango mkubwa wa Maendeleo ya jamii hivyo ni vema kwa Viongozi na Waumini kuwa Mstari wa mbele kuhubiri Amani ili Serikali ifanye Jukumu la Kuleta maendeleo kwa Ufanisi.
Rais Dk.Mwinyi ameeleza kufarijika na mchango unaotolewa na KKKT ya jamii hususan katika masuala ya Afya, Elimu, Maji na Malezi ya Yatima na Kuwasisitiza kuendelea na michango hiyo ambayo imekuwa msaada mkubwa kwa jamii.
Halikadhalika Rais Dk.Mwinyi amelishauri Kanisa hilo kuwekeza katika sekta ya utalii, elimu, biashara na uwekezaji na Serikali iko tayari kushirikiana nao na kutoa kila msaada kufanikisha azma hiyo.
Vilevile Rais Dk.Mwinyi amepongeza juhudi za Kanisa kuwaendeleza vIjana kielimu kupitia Chuo Kikuu cha Tumaini kwa Mafunzo mbalimbali na kuchangia kuzalisha Wataalamu Wazalendo pamoja na kuwa na wazi la kuanzisha Tawi la Chuo hicho Zanzibar.
Naye Askofu Alex Malasusa ambae pia ni Mkuu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani ameshukuru Ushirikiano Uliopo baina ya Serikali na Kanisa hilo aliouelezea kuwa ni kichocheo cha mambo yote ya Maendeleo yanayaofanywa na Kanisa pamoja na kupongeza hatua za Maendeleo katika Ujenzi wa Miundombinu, Ubunifu na utekelezaji wa Sera ya Uchumi wa Buluu kwa Mafanikio na kudumisha amani na utulivu nchini.