Mjumbe wa Halmashaur Kuu ya CCM Dkt. Doto Biteko ambaye ni Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati ameonya uwepo wa makundi ndani ya chama hicho kuelekea uchaguzi badala nguvu kubwa ielekezwe kwenye kujenga umoja na kutowapa nafasi wapinzani.
Dkt. Biteko amesema hayo katika mkutano wa Jimbo la Chamwino ulioendana na uwasilishaji wa utekelezaji wa Ilani ya CCM katika kipindi cha maka mitano ya mbunge wa Jimbo hilo Deogratius Ndejembi ambayo pia n Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
“Uchaguzi unaokuja ni uchaguzi usiokuwa wa majaribio ni uchaguz unaotaka kuungana kwa pamoja na tulivyo weng tunaweza tukawa na tofauti mbalimbali na misimamo ya aina tofauti niwaombe tuache tofauti zetu tukitazame chama tushikamane kwa pamoja hatuna sababu ya kuhangaika kuwazungumza wengine tuzungumze mambo tuliyonayo ndani ya chama chetu” Dkt. Doto Biteko
Dkt. Biteko ameongeza kuwa “Nchi yetu ina vyama vingi vya siasa vina kazi mbili na chama kimoja kina kazi ya kufanya na chama kingine kinakazi ya kusema nyie wanaCCM fanyeni kazi hivyo vyama vingine viachieni maneno yas kusema wananchi watawapima kwa kazi sio kwa maneno ya kusema”