Eldiara Doucette, Mwanamke mwenye umri wa miaka 22 kutoka Marekani, amefanya mazishi ya kipekee kuuaga mkono wake wa kulia alioupoteza baada ya kukatwa kutokana na Saratani ya synovial sarcoma .
Aina hii nadra ya Saratani inayoshambulia tishu laini iliushambulia mkono wake na alifanyiwa upasuaji wa kuukata.
Eldiara alikusanya Familia yake, Mpenzi wake na Marafiki zake wa karibu ili kusema kwaheri kwa mkono wake huo alioupoteza baada ya kufanyiwa upasuaji wa kukatwa kwa sababu ya uvimbe uliosababishwa na Ugonjwa wa Saratani.
Katika sherehe hiyo Eldiara alivalia mavazi meusi na kukaa kando ya mkono wake aliyouikwa akiushukuru kwa kazi ulizofanya kwa miaka 22 pia ameandika kwenye Instagram kuwa ingawa saratani imechukua mkono wake ameona kama vile mkono wake umejitoa sadaka kwa ajili ya maisha yake.