Rais wa Marekani, Donald Trump alisema Jumatatu kwamba hawezi kutoa hakikisho la kusitishwa kwa mapigano makali katika Ukanda wa Gaza unaozingirwa kutafanyika, siku moja tu kabla ya kumkaribisha Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu katika Ikulu ya White House.
Trump aliwaambia waandishi wa habari katika Ofisi ya Oval kwamba “hana hakikisho” kwamba makubaliano yatasalia kutekelezwa.
“Nimeona watu wakitendewa unyama. Hakuna mtu aliyewahi kuona kitu kama hicho. Hapana, sina uhakika kwamba amani itadumu,” alisema.
Trump atakuwa mwenyeji wa Netanyahu siku ya Jumanne katika ambayo itakuwa ni ziara ya kwanza rasmi ya kiongozi wa kigeni tangu ashike madaraka mwezi uliopita.