Alphonso Davies amesaini mkataba mpya na Bayern Munich, utakaomweka katika klabu hiyo hadi 2030. Licha ya kutakiwa na Real Madrid, mchezaji huyo wa kimataifa wa Canada ameweka mustakabali wake kwa wababe hao wa Bavaria.
Beki huyo wa kushoto mwenye umri wa miaka 23, ambaye mkataba wake wa awali ulikuwa unamalizika 2025, amekuwa mtu muhimu kwa Bayern tangu ajiunge na klabu hiyo mwaka 2018.
“Nina furaha sana kuongeza mkataba wangu katika klabu hii kubwa,” alisema Davies. “Nilikuja Bayern nikiwa na miaka 18 na nilitaka tu kujifunza kila siku ili kuwa mmoja wa bora katika nafasi yangu. Sasa, ninatazamia miaka mingine mitano.”
“Nilikuja FC Bayern nikiwa na umri wa miaka 18 na nilitaka tu kujifunza mengi iwezekanavyo kila siku ili kuwa mmoja wa wachezaji bora katika nafasi yangu. Sasa natazamia miaka mingine mitano pamoja.
Tayari nimepata mengi hapa, lakini kuna mengi yanakuja.”