Kundi la waasi la Machi 23 (M23) na wanajeshi wa Rwanda wameanzisha mashambulizi mapya mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) siku ya Jumatano, Februari 5, kuelekea Bukavu, mji mkuu wa mkoa huo. Baada ya kuchukua Goma, mji mkuu wa mkoa jirani wa Kivu Kaskazini, Januari 27, M23 ilitangaza kwa upande mmoja usitishaji mapigano kwa sababu za kibinadamu ambao ulipaswa kuanza kutekelezwa tarehe 4 Februari.
Kundi hili la wasi liliongeza kuwa “halina nia ya kuchukua udhibiti wa mji wa Bukavu au maeneo mengine
Kundi hilo linaloipinga serikali na wanajeshi wa Rwanda walianzisha mapigano makali alfajiri dhidi ya wanajeshi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (FARDC) huko Kivu Kusini, duru za usalama na mashirika ya kutoa misaada ya kibinadamu zimeiambia shirika la habari la AFP.
Waliteka mji wa uchimbaji madini wa Nyabibwe, takriban kilomita 100 kutoka Bukavu na kilomita 70 kutoka uwanja wa ndege wa mkoa.
“Huu ni uthibitisho wa wazi kwamba usitishaji vita wa upande mmoja ambao ulitangazwa, kama kawaida, ulikuwa udanganyifu,” msemaji wa serikali ya Kongo Patrick Muyaya ameliambia shirika la habari la AFP.