Ashton Mann kutoka Kearns, Utah Nchini Marekani amekamatwa kwa tuhuma za kumuua Rafiki yake bila kukusudia baada ya kujaribu kuthibitisha kauli ya Rafiki yake kwamba anaweza kukwepa risasi.
Taarifa inaeleza kuwa tukio hilo limetokea wakati wawili hao walipokuwa wakicheza na bunduki ambapo Rafiki wa Mann alidai kuwa ana uwezo wa kukwepa risasi.
Kwa bahati mbaya walipokuwa wanacheza Bunduki ilifyatuka risasi na kumgonga Rafiki yake kifuani na kupeleka kifo chake.
Kwa mujibu wa taarifa za Polisi Mann amekamatwa na kufikishwa Mahakamani huku tukio hilo likitoa tahadhari kwa jamii kuhusu hatari ya kutumia silaha bila tahadhari na umuhimu wa kuwa makini.