Marcus Jordan Mtoto wa aliyekua Gwiji wa Mpira wa kikapu Michael Jordan, amekamatwa huko Florida kwa tuhuma za kuendesha Gari akiwa amelewa na kumiliki dawa za kulevya aina ya cocaine ambapo Polisi walimkamata baada ya kugundua Gari lake aina ya Lamborghini limekwama kwenye reli za treni na uchunguzi wa awali ukaonesha dalili za ulevi pamoja na umiliki wa dawa hizo haramu.
Kwa mujibu wa taarifa za Polisi Marcus alikataa kushirikiana na Maafisa wa usalama wakati wa ukamataji hali iliyosababisha kuzuiliwa kwake mara moja na upekuzi wa Gari lake ulizua ushahidi wa uwepo wa cocaine ambapo kwa sasa anashikiliwa akisubiri kufikishwa Mahakamani.
Rekodi zinaenesha kuwa hii si mara ya kwanza kwa Marcus kukumbwa na matatizo ya kisheria kwani mwaka 2012 alikamatwa kwa utovu wa nidhamu na kupinga kukamatwa akiwa amelewa lakini pia mwaka jana alihusishwa na video inayodaiwa kumuonesha akitumia dawa haramu wakati wa mapumziko yake alipokuwa huko Ufaransa jambo lililozua mjadala miongoni mwa Mashabiki wa Familia ya Jordan.
Hata hivyo Kufuatia kukamatwa kwake bado hakuna tamko rasmi kutoka kwa Familia ya Jordan huku wengi wakisubiri hatua za kisheria zitakazochukuliwa dhidi yake.