Wasichana na wanawake waliobadili jinsia hawatashindana tena katika hafla za michezo kike na katika hafla nyingi za michezo za vyuo vikuu nchini Marekani hii ni baada ya uamuzi wa baraza linaloongoza michezo kuwazuia wanariadha ambao walikuwa wanaume hapo awali na kubadili jinsia.
Chama cha Kitaifa cha Wanariadha wa Vyuo Vikuu, bodi kuu inayosimamia michezo ya vyuo vikuu nchini Marekani, ilisema Alhamisi kwamba itapunguza ushindani katika michezo ya wasichana na wanawake kwa wanariadha waliozaliwa na wanawake pekee.
Tangazo la NCAA linakuja baada ya Rais wa Marekani, Donald Trump kutia saini amri ya utendaji siku iliyotangulia ya kunyima ufadhili wa taasisi za elimu zinazoruhusu wasichana na wanawake kushiriki katika mashindano ya michezo ya kike.
“NCAA ni shirika linaloundwa na vyuo na vyuo vikuu 1,100 katika majimbo yote 50 ambayo kwa pamoja yanasajili zaidi ya wanariadha wanafunzi 530,000.
Tunaamini kwa dhati kwamba viwango vya ustahiki vilivyo wazi, thabiti na vinavyofanana vitasaidia vyema zaidi wanariadha wanafunzi wa siku hizi badala ya viraka vya sheria zinazokinzana za serikali na maamuzi ya mahakama,” rais wa NCAA, Charlie Baker, alisema katika taarifa.
“Kwa maana hiyo, agizo la Rais Trump linatoa kiwango cha wazi cha kitaifa kuhusu ubadilishaji jinsia”