Rais wa Jamhuri ya Uganda, Mhe. Yoweri Kaguta Museveni amewasili nchini Tanzania na kupokelewa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, leo tarehe 08 Februari 2025
Rais Museveni atashiriki Mkutano wa Dharura wa Pamoja Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) utakaofanyika leo.
Jumuiya zote mbili zinakutana kwa pamoja kujadili kwa lengo la kupatia ufumbuzi hali ya ulinzi na usalama katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.