Donald Trump alisema anabatilisha kibali cha usalama cha Rais wa zamani Joe Biden na kumaliza taarifa za kijasusi za kila siku anazopokea.
Aliongeza – katika chapisho kwenye ukurasa wake wa Truth Social kuwa alifanya hivyo sababu ilikuwa malipo kwa Bwana Biden kumfanyia vivyo hivyo mnamo 2021.
Bw Trump pia alirejelea ripoti ya Wakili Maalum Robert Hur iliyomtaja Bw Biden mwaka jana kama “mzee mwenye nia njema na asiye na kumbukumbu nzuri”.
Marais wa zamani kwa kawaida hupokea taarifa za kijasusi hata baada ya kuondoka madarakani.
Mnamo 2021, muda mfupi baada ya kuingia madarakani, Rais Biden aliiambia CBS kuwa haamini kuwa Bw Trump anafaa kupata taarifa za kijasusi kwa sababu ya “tabia yake mbaya” na wasiwasi kwamba anaweza kushiriki habari.
Siku ya Ijumaa, Trump aliandika kuhusu uamuzi wake wa kufanya vivyo hivyo.
“Yeye [Biden] aliweka mfano huu mnamo 2021, wakati aliamuru Jumuiya ya Ujasusi (IC) kumzuia Rais wa 45 wa Marekani(ME!) kupata maelezo juu ya Usalama wa Kitaifa, heshima iliyotolewa kwa Marais wa zamani.