Rais wa Marekani Donald Trump alisema Jumapili kwamba anaamini Marekani inapiga hatua katika mazungumzo yake ya kumaliza vita kati ya Urusi na Ukraine, lakini alikataa kutoa maelezo kuhusu mawasiliano yoyote aliyokuwa nayo na Rais wa Urusi Vladimir Putin.
Akizungumza na wanahabari ndani ya Air Force One, Trump alidokeza kuwa watu hao wawili walikuwa wakiwasiliana; hayo yatakuwa mazungumzo ya kwanza kutambuliwa rasmi kati ya Putin na rais wa Marekani tangu mapema 2022.
Alipoulizwa kama alikuwa na mazungumzo yake na Putin tangu awe rais Januari 20 au kabla, Trump alisema: “Nimekuwa nayo. Wacha tuseme nimekuwa nayo … Na ninatarajia kuwa na mazungumzo mengi zaidi. Tunapaswa kumaliza vita hivyo.”
“Ikiwa tunazungumza, sitaki kukuambia juu ya mazungumzo,” Trump alisema. “Naamini tunapiga hatua. Tunataka kusimamisha vita vya Ukraine na Urusi.”
Rais alisema Marekani inawasiliana na Urusi na Ukraine. “Tunazungumza na pande zote mbili,”tutayamaliza alisema