Hali mbaya ya hewa huko Gaza inazidisha masaibu na maafa ya Wapalestina katika Ukanda huo.
Kufikia jana, njia muhimu mbili kupitia kinachojulikana kama Ukanda wa Netzarim zilifunguliwa na wengi walionekana wakirudi kwenye nyumba zao kaskazini mwa eneo hilo.
Wengi wanaumia sana kurudi bila kitu. Hakuna chochote kilichosalia kwao katika suala la majengo ya makazi, vituo vya umma au hata makao ya muda ili kuwalinda kutokana na hali ya hewa.
Hasa, tangu asubuhi ya leo, mvua kubwa, ikifuatiwa na upepo mkali, imepeperusha mahema mengi yaliyowekwa katika eneo tulipo.
Mengi ya maeneo hayo yalipojengwa mahema yamekuwa maeneo ya wazi baada ya majengo ya makazi kugeuzwa vifusi.
Na kukosekana kwa majengo kumeunda ombwe hapa kwa upepo kuwa na nguvu zaidi na mvua kunyesha kwa njia tofauti.
Hii inasababisha mitaa kujaa maji na matope.