Mamlaka ya mapato Tanzazi TRA imewataka wateja wake kulipa kodi kwa wakati ili kuondokana na kupigwa faini kwani mteja akichelewa kulipa kodi
atakutana na riba jambo ambalo si zuri kwa mfanyabiashara
Hayo yamesemwa na meneja Elimu kwa mlipakodi kutoka TRA Paul John
Walalaze katika utoaji elimu kwa na tasisi zisizo za kiserikali (Ngo’s) ziolizopo mkoani Singida hii ikiwa ni maelekezo kutoka kwa kamishna mkuu wa TRA kutoa elimu juu ya kulipa kodi.
Naye afisa mkuu msimamizi wa kodi kutoka TRA Hamad Mtery amesema kuwa Taifa l Tanzania limepitisha mapato za aina tatu ambayo ni mapato yatokanayo
na Ajira, mapato yatokanayo na biashara na mapato yatokanayo na uwekezaji hivyo makundi yote yanatakiwa kujisajili ili kuanza kulipa kodi na kufanya shughuli zao kihalali