Maafisa wakuu wa Marekani na Urusi wanatazamiwa kukutana nchini Saudi Arabia kwa kile kinachotarajiwa kuwa mazungumzo muhimu zaidi kufikia sasa juu ya kumaliza vita nchini Ukraine.
Tutakuwa na maelezo zaidi kuhusu ni nani tunayetarajia kuwa kwenye mkutano huko Riyadh baada ya muda mfupi – lakini inafikiriwa kuwa mazungumzo hayo yanaweza kufungua njia ya mkutano wa kilele kati ya Donald Trump na Vladimir Putin katika wiki zijazo.
Inafuatia simu kati ya viongozi hao wawili wiki iliyopita, ambapo walikubaliana kuanzisha mazungumzo ya kumaliza vita.
Mazungumzo hayo yamezua wasiwasi nchini Ukraine na kote Ulaya kwamba wanaondolewa kwenye mazungumzo, na kusababisha mkutano kati ya viongozi mjini Paris jana.
Viongozi wa Ulaya waliahidi kuwekeza zaidi katika ulinzi na kuongoza katika kutoa dhamana ya usalama kwa Ukraine.