Naibu waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na uwekezaji Stanslaus Nyongo akimwakilisha Waziri wa Fedha katika kuzindua Ofisi ya Hazina ndogo yenye thamani ya zaidi ya Bilioni 4 wilayani Geita Mkoani humo amezitaka Taasisi za Kifedha nchini kuacha mara moja kukopesha fedha kwa riba kubwa na badala yake wafuate utaratibu.
Akizungumza Mara baada ya kuzindua jengo hilo Naibu waziri Nyongo amesema utoaji wa riba kubwa kwa mikopo binafsi umekuwa ukipelekea kurudisha nyuma maendeleo ya wananchi huku akizitaja baadhi ya mikopo ambayo imekuwa sugu na janga kwa wananchi ikiwemo mikopo ya kausha damu , mikopo umiza , mikopo kuzimia .
” Ndugu zangu wageni waalikwa wanageita wenzangu pamoja na mafanikio haya kumekuwa na changamoto mbalimbali katika sekta ya fedha ikiwemo utoaji wa mikopo yenye riba kubwa inayowaumiza wananchi na kuwarudisha nyuma kimaemdeleo ambayo mikopo hii inajulikana kwa jina maarufu kama mikopo umiza, mikopo kausha damu , mikopo kuzimia mikopo chuma hulete nk , ” Mwakilishi wa waziri wa Fedha , Stanslaus Nyongo.
“Natoa onyo kwa watu binafsi na kampuni zinazo jihusisha na utoaji wa mikopo ya namna hii kuacha mara moja kwani jambo hili linarudisha nyuma wqnanchi wetu kiuchumi na kuwaingiza katika limdi la umasikini aidha nawakumbusha wananchi wote kuwa na nidhamu ya fedha ikiwemo kukopa kwa ajili ya mahitaji yenye tija na ikiwezekana kuchukua mikopo kwa ajili ya shughuli za uzalishaji Mali badala ya matumizi ya kawaida , Mwakilishi wa waziri wa Fedha , Stanslaus Nyongo.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Geita akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Geita Hashim Komba amempongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuleta fedha hizo kwa ajili ya ujenzi wa ofisi hiyo na kwa namna ambavyo amekuwa akileta fedha za ujenzi wa miundombinu mbalimbali ndani ya wilaya ya Geita .
” Leo hii tunaangalia kazi hii njema ya jengo kubwa ambalo tunaenda kufanya uzinduzi watani zangu wasukuma toka wamekuja hapa nilikjwa napokea taarifa zao Mh Naibu waziri ni watani zangu tumetumia kazi kubwa sana kuwazuia wasije kupiga vitu kwa namna ambavyo jengo ni zuri , ” Mwakilishi Mkuu wa Mkoa wa Geita , Hashim Komba.
” Mheshimiwa Mgeni rasmi tarehe ya kuanza mradi huu ilikuwa ni tarehe 30 Juni 2023 na tarehe ya kukabidhi 3 , Disemba 2024 mradi huu ni mradi wa miezi 15 na ghalama za mradi ni bilioni 4 milioni 37, 98432.95 pamoja na VAT , ” Mshauri Elekezi TBA , Amona Lumuli.