Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe Dkt. Selemani Jafo (Mb.) ameliagiza
Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) kukamilisha majadiliano na Mwekezaji wa Mradi wa Makaa ya Mawe Ketawaka Kampuni ya MM Steel Resource Public Ltd( MMSR) kufikia makubaliano ndani ya wiki tatu ili utekelezaji wa Mradi huo uanze.
Vilevile, Waziri Jafo ameliagiza Shirika hilo kushirikiana na Wadau wake mbalimbali katika Mradi wa Makaa ya Mawe Mchuchuma na Katewaka kujenga majengo mawili katika Shule ya Msingi Nkomang’ombe iliyopo katika maeneo ya Miradi hiyo.
Waziri Jafo ametoa agizo hilo wakati wa ziara yake Mkoani Njombe katika Wilaya ya Ludewa yenye lengo la kukagua maendeleo ya utekelezaji wa Mradi Mchuchuma na Ketawaka, Liganga na Maganga Matitu pamoja na kuongea na Wananchi wa maeneo hayo.
Akiongea na Wananchi wa Kijiji cha Nkomang’ombe, Waziri Jafo amewahakikishia kuwa atashurukiana nao kuhakikisha Mtafi huo unaanza kutekrlrzwa ili kutumiza malengo ya Serikali ya Awamu ya Sita, kuongeza ajira na Pato la Taifa kwa ujumla.
Awali Afisa Mradi wa NDC Bw. Wallu Kapaya akitoa Taarifa ya utekelezaji wa Mradi wa Ketawaka amesema Mradi huo una tani milioni 100 za makaa ya mawe utakaapoqnza uchimbaji una uwezo wa kuzalisha tani milioni 1.5 kwa mwaka na unatarajiwa kudumu kwa miaka 100 huku ukitoa ajira 1000 ambapo ajira za moja kwa moja 250