Kamati ya kudumu ya bunge ya uwekezashaji wa mitaji ya umma, Imefanya ziara mkoani Arusha ikitembelea minara ndani ya wilaya ya Monduli katika kata ya sepeko na Esilalei kwa lengo la kukagua mradi mkubwa wa Tanzania kidijitali unao fanya ujenzi wa minara 758 inayogaribu zaidi ya bilioni 126 itakayotekelezwa ndani ya mikoa 26 na kunufaisha kata 713 nchi nzima na kuwawezesha huduma ya mawasiliano watanzania zaidi ya milioni nane na laki nane.
Akikagua Minara hiyo Agustino Hollei mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge ya uwekezaji wa mitaji ya umma, akaeleza kuridhishwa na mradi huo umefanikiwa kukamilika kwa asilimia 52 huku asilimia zilizo baki zikitarajiwa kukamilika hadi ifikapo Mei mwaka huu huku akitoa rai kwa wa kandarasi kuwa hawatoongeza muda ili kukamilisha miradi huo hivyo kujitahidi kukamilisha kwa wakati ulio pangwa.
Aidha Mkurugenzi wa uendeshaji katika mfuko wa mawasiliano kwa wote (UCSAF) Richard….ameelezachangamoto mbalimbali zinazo kabiliwa utekelezwaji wa mradi ikiwemo barabara kutofikika licha ya serikali kutoa vibali vya muda ili kuwawezesha watoa huduma wote kuanza ujenzi hivyo kuwataka watoa huduma kuhakikisha kazi inakamilika kwa wakati
Ikiwa kwa kanda ya kaskazini inatarajiwa kusambazwa minara 141 Wananchi wa kata ya sepeko na Esilalei wilayani Monduli mkoani Arusha waliofikia na mradi huo wakaeleza manufaa wanayopata pamoja baada ya minara kuwasha kwani walikuwa wakikabiliwa na changamoto na kutokuwa na mtandao kwa muda mrefu