Kundi la Hamas limekabidhi miili ya mateka wanne waliouawa na Israel katika shambulio la bomu huko Gaza kwa shirika la Msalaba Mwekundu, kwa mujibu wa TRT World.
Shirika la Msalaba Mwekundu lilielekea eneo la Gaza kupokea miili 4 ya mateka wa Israel walioratibiwa kukabidhiwa chini ya makubaliano ya kusitisha mapigano, vyombo vya habari vya Israel vimeripoti.
Kurejeshwa kwa miili hiyo kulifanyika katika mji wa kusini wa Gaza wa Khan Younis.
Kabla ya uhamisho huo mamia ya watu walikusanyika karibu na eneo lenye mchanga ambalo hapo awali lilikuwa likitumika kama kaburi. Uzio ulikuwa umewekwa ili kuwaweka watazamaji mbali na eneo la karibu ambapo makabidhiano ya Msalaba Mwekundu yangefanyika.
Hamas ilionesha majeneza 4 meusi kwenye jukwaa huko Gaza kabla ya kukabidhiwa miili ya mateka.
Hamas ilisema itakabidhi miili ya Shiri Bibas, Kfir, Ariel, na Oded Lifshitz.